*VIDONDA VYA TUMBO*, au *GASTRIC ULCERS*, ni majeraha yanayotokea kwenye ukuta wa ndani wa tumbo.
🌳Husababishwa na kushuka kwa kiwango cha ute (mucus) unaolinda kuta za tumbo dhidi ya asidi kali inayozalishwa kwa ajili ya kumeng'enya chakula.
🌳Hali hii hufanya sehemu za kuta za tumbo kuwa wazi na kuathirika, na hivyo kusababisha majeraha au vidonda.
*Hizi ni dalili za vidonda vya tumbo (Gastric Ulcers):-*
👉 Maumivu makali ya tumbo, hasa sehemu ya juu.
👉 Kiungulia (hali ya kuchomachoma kifuani).
👉 Kichefuchefu na kutapika.
👉 Kutapika damu au kutapika vitu vyenye rangi ya kahawia.
👉 Kinyesi chenye rangi nyeusi au kinachoonekana kama lami.
👉 Kupoteza uzito bila sababu maalum.
👉 Kukosa hamu ya kula.
NB: Vidonda vya Tumbo vikikaa kwa muda mrefu bila matibabu kamili, vinaweza kupelekea Kansa/ Cancer ya Tumbo

0 Comments